Msanii maarufu Kabi wa Jesus ambaye alivuma sana kwa wimbo wake wa ‘Thithima’ na mkewe Milly wamejaliwa mtoto wa kiume

Wawili hao walitangaza habari hizo njema kupitia mitandao ya kijamii ambapo pia waliwajuza wafuasi wao kuhusu safari yao katika ndoa.

Habari Nyingine: Moses Kuria akosoa Matiang’i kwa kutangaza sikukuu ya Moi

Kabi na Milly waliwashukuru wafuasi wao kwa kusimama nao katika kila hali na kuahidi kwamba watakuwa wakiwajuza kila kitu wanapoanza kumlea mtoto wao wa kwanza.

” Tunashukuru Mungu kwa kutubariki na mtoto wetu wa kwanza, pia tunawashukuru wafuasi wetu kwa kusimama nasi,” Wawili hao waliandika Instagram.

Habari Nyingine: Afya yako: Fahamu kuhusu maumivu ya kabla na wakati wa hedhi

” Safari ya ujauzito imekuwa njema, tunashukuru kwa wale waliotujali wakitaka kujua ni vipi tulikimya kwa muda wa juma moja bila kutoa video au kuchapisha picha zozote mitandaoni, hii ni kwa sababu tulikuwa tunasubiri kumkaribisha mtoto wetu,” Waliongezea.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here