Aliyekuwa baunza wa mwanamuziki staa wa Bonge Fleva Diamond Platnumz Mwarabu Mirundi almaarufu Mwarabu Fighter amefunguka mengi kuhusu maisha yake ya sasa na yale maisha aliyokuwa akiishi wakati akichapa kazi WCB.

Wakati akihojiwa na mtandao wa Bongo5 Mwarabu Fighter alisema kuwa aliondoka kwa Diamond Platnumz almaarufu Chibu bila kitu ingawa alijitolea kila wakati kumlinda msanii huyo na jina lake kubwa.

Habari Nyingine: Shabiki aikwamia suti ya Harmonize jukwaani wakati akimtumbuiza Rais Magufuli

” Nilipoacha kazi nilihangaika sana maana sikuwa na hata senti mia, mke wangu aliuza genge mtaani ili tupate chochote, vijana wengi wajifunze kupitia kwangu. mimi niliishi ili kulinda Brand ya Diamond hali ya kuwa mfukoni sina kitu, niliishi ili niendane na Brand ya msanii mkubwa lakini katika nafsi yangu niliumia sana,” Mwarabu alisema.

Habari Nyingine: Otile Brown akataa kuwachika, amuomba mpenziwe wa zamani kumkubali

Katika mahojiano hayo ambayo TUKO.co.ke imeyasikiliza kwa makini, mkamambe huyo anasema kuwa, wakati huo hakuwa na gari wala pikipiki wala chombo chochote cha usafiri lakini alikuwa apanda magari ya kulipia.

Habari Nyingine: Nusura Ronaldo ajiunge na Arsenal 2003, afunguka na kusema pole kwa Arsene Wenger

“Mshahara wangu haukutosha hata kwa wiki mbili lakini sikuwa na namna” Mwarabu aliongeza

Mbali na hilo mwarabu alifunguka kuhusu kuzungumziwa na kuimbwa kwenye nyimbo na wasanii kutoka lebo WCB ambayo ipo chini ya Diamond.

Kulingana naye, Chibu kwenye wimbo wake wa Inama na ule wa Harmonize akimshirikisha Q Chillah ‘My Boo’ kuhusiana na mpenzi wa Harmonize Sarah, wanafahamu nini kilichotokea.

Habari Nyingine: Mume wa zamani wa Wangari Maathai afariki dunia

“Ukweli wanao wao Diamond Platnumz anaujua ukweli lakini pia Harmonize anaujua ukweli, wao wanatumia nyimbo zao kufikisha ujumbe lakini hawataki kuongea ukweli, mi nafurahi wanavyoniongelea kwani bado wanakumbuka makubwa niliyowafanyia” alisema.

Kabla ya kuondoka WCB, kulikuwapo na madai mengi kuwa, Mwarabu alikuwa akitoka kimapenzi na Sarah.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here